Mambo Kumi na Mawili Ambayo Wazazi Wanaweza Kufanya Ili Kuzuia Uraibu
Zana hii inaelezea mikakati ya uzuiaji kwa njia rahisi ambayo wazazi na walezi wanaweza kujumuisha katika maisha ya kila siku, ili kufanya tuwezalo kuwalinda watoto wetu dhidi ya uraibu baadaye maishani.
Uraibu ni hali ya kiafya inayoathiri ubongo na kubadilisha tabia ya mtu. Neno la kimatibabu la uraibu wa dawa za kulevya au pombe ni tatizo la matumizi ya vileo.
Kuna sehemu kuu mbili za ubongo zinazoathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya: mfumo wa ubongo unaochochea hisia na koteksi. Mfumo wa ubongo unaochochea hisia, ulio kilindini mwa ubongo, huhusika katika silika zetu za kimsingi za kustahimili. Koteksi ni kitengo cha maamuzi na udhibiti wa msukumo.
Jinsi ya Kufanyia Mazoezi Stadi ya Kukataa
Fanya mazoezi ya utumaji ujumbe muhimu ambao vijana wanaweza kutumia katika hali hatari. Kwa mfano, mazungumzo kuhusu jinsi ya kukabili msukumo kutoka kwa wanarika wenzao au watu wengine kunywa au kutumia dawa za kulevya kwa kutoa majibu mahususi yanaweza kusaidia kuwatayarisha vijana kukabiliana na hali hizo. Kuna aina tano tofauti za ujuzi wa kukataa. Fanyia mazoezi ya chaguo zinazokufaa zaidi. Kijana wako aliyebaleghe anaweza kuigiza au kuandika majibu ambayo yanafaa zaidi.
Matumizi ya opiodi huathiri sehemu muhimu ya ubongo ambayo hudhibiti ufanyaji wa maamuzi, kujidhibiti na mchakato wa kujipa raha.